Seventh-day Adventist® Church

Sinza, Dar es salaam, Tanzania Kanisa la Waadventista Wa Sabato Sinza

Menu
Add a Slideshow to see your custom images here
Waadventista wasabato huipokea Biblia kama kanuni yao pekee na hushika baadhi ya misingi ya imani kuwa ndiyo mafundisho ya mabadiliko matakatifu. Imani hizi, kamazilivyoorodheshwa hapa, hufanya welekevu wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho ya mabadiliko. Masahihisho ya kauli hizi yanaweza kutegemewa katika kikao cha Halmashaurikuu wakati kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye ufahamu ulio kamili zaidi ya ukweli wa Biblia au linapopata lugha iliyo bora zaidi ya kuelezea mafundisho ya Neno Takatifu la Mungu.

1.Maandiliko Matakatifu 
Maandiko Matakatifu, yaani Agano la kale na Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu walionena na kuandika kamawalivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya mungu katika historia. (2Petro 1:20,21. 2Timotheo 3:16,17. Zaburi 119: 105. Mithal 30: 5,6. Isaya 8:20. Yoh 17:17. 1Wathe 2:13. Waeb4:12.)

2.Utatu Mtakatifu 
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele. Mungu hapatikani na mauti, mwenye nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko daima. Yeye hana mwisho na ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika kupitia kujifunua kwake binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, kutumikiwa na viumbe vyote. (kumb 6:4. Mith 28:19. 2kor 13:14. Waef 4:4-6. 1Petr 1:2 1Tim 1:17 Ufunuo 14:7)

3.Baba
Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji, Chimbuko, Mtengenezaji, na Mfalme wa viumbe wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, Mwingi wa rehema,, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba. (Mwanzo 1:1 Ufu 4:11.
1wakor 15:28. Yoh 3:16. 1Yoh 4:8. 1Tim 1:17. Kut 34:6,7. Yoh 14:9).

4.Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanya mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote viliumbwa, tabia ya mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakaribishwa na ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu alioonyesha kwa mfano wa haki na u[endo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, Alifufuliwa kutoka kwa wafu, na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika utukufu kwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh 1: 1-3,14. Wakol 1: 15-19,. Wafil 2:5-11. Yoh 10:30, 14:9 Warum 6:23. 2Wakor 5:17-19.Yoh 5:22. 1Wakor 15:3,4. Luka 1:35. Yoh 14:1-3)

5.Roho Mtakatifu 
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji, kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu. Alijaza maisha ya kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa, huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko uliongoza kwenye ukweli wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2Petr 1:21. 2Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26, 15:26,27, 16:7-13)

6.Uumbaji 
Mungu ni muumba wa vitu vyote, na amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio la
shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “Mbingu na Nchi” na vitu vyote
vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo
akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji.
Mwanaume na Mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa
kazi yake ya Uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuajibika na
utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana”
ukitangaza utukufu wa Mungu. (Mwa 1,2. Kut20:8-11. Zab 19:1-6, 33:6-9, 104. Waebr
11:3)

7.Asili ya Mwanadamu 
Mwanaume na Mwanamke walifanyawa kwa mfano wa Munguwakiwa kila mmoja na nafsi
yake, uwezo na uhuru wa kufikirina kutenda. Ingawa waliumbwa viumbe huru, kila mmoja
ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili, akili na roho, akimtegemea Mungu kwa uhai na
pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana
utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka kutoka hadhi yao ya juuchini ya Mungu. Sura
ya Mungu iliyopo ndani yao ikaharibika na wakawa chini ya mauti. Wazao wao hushiriki
asili hii ya kuanguka na matokeo yake. Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya
kuelekea kwenye uovu. Lakini Mungu katika kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake,
na kwa Roho wake hurejesha ndani ya mwanadamuwatubuo sura ya muumba wao.
Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu, wanaitwa kumpenda na kupendana
wao kwa wao na kutunza mazingira yao.(Mwa 1:26-28, 2:7. Zab 8:4-8. Mdo 17:24-28. Mwa
3. Zab 51:5 War 5:12:17. 1Yoh 4:7,8,11,20. Mwa 2:15

8.Pambano kuu 
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina ya kristo na shetani
kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya ulimwengu. Ugomvi huu
ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua, katika
kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na kupelekea sehemu ya Malaika kwenye uasi.
Akaiagiza Roho ya uasi katika ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa

kingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji ya sura ya
Mungukatika wanadamu, Uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea
wakati wa gharika iliyokumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote ulimwengu
huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo
hatimaye akathibitika kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano
hili, kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na
kutegemeza katika njia ya wokovu. (Ufu 12:4-9, Isa 14:12-14, Eze 28:12-18, War 1:19-32,
5:12-21, 8:19-22, 1Wakor 4:9, Waeb 1:14)

9.Maisha, Mauti na Ufufuo wa kristo 
Katika maisha ya kristo ya utii mtakatifu kwa mapenzi ya Mungu, mateso yake, mauti na
ufufuo, Mungu alitoa njia pekee ya kafara kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu, ili kwamba
wale ambao kwa imani wanapokea upatanisho huu waweza kuwa na uzima wa milele, na
ulimwengu wote uweze kuelewa vizuri upendo mtakatifu usio na kikomo wa muumba.
Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya mungu na fadhili za tabia yake, kwa
sababu hufanya vyote viwili kuhukumu dhambi zetu na kutupatia msamaha. Kifo cha kristo
ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na chenye kubadilisha. Ufufuo wa Yesu kristo
hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu, na kwa wale wanaopokea kafara
huakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya dhambi na mauti. Kinatangaza ukuu wa Yesu
Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni na duniani litapigwa.(Yoh3:16, Isa13:1,
1Petr 2:21, 22,1Wakor 15:3, 4, 20-22, 2Wakor 5:14, 19-21. War1:4, 3:25, 4:25, 8:3, 4,
Wafil2:6-11)

10.Uzoefu wa Wokovu 
Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya Kristo, asiyejua dhamdi
kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwambakatika yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu.
Tukiongozwa na Roho mtakatifu tunatambua hitaji letu, tunakili hali yetu ya kuwa wenye
dhambi, tunatubu maasi yetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo,
kama mbadala na kielelezo. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa
kimbingu wan a ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa kristo tunahesabiwa haki,
tunafanywa kuwa wana wa binti za Mungu, na kukomesabiwa haki kutoka katika hali ya
kuwa chini ya dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upyana kutakaswa, Roho hufanywa
upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo
wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washiriki wa asili ya uungu na
tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu. (2Wakor 5:17-21, Yoh3:16, Wag1: 4, 4:4-
7, Tito3:3-7, Yoh16:8, Wag3:13,14. 1Petr 2:21,22. Warumi10:17, 3:21-26, 8:14-17, 12:2.
Warumi8:1-4,5:6-10, 2Petr 1:3,4)

11.Kukua katika kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo
wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha
mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya nguvu
za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, fyraha, na
uhakika wa upendo wake.Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu.
Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa
huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya
nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika
uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea
naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa ajili
ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo
wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia
ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho. (Zab.1:1,2. 23:4, 77:11,12,
Kol1:13-14, 2:6, 14-15, Luka10:17-20, Efe5:19-20, 6:12-18, 1Theo 5:23, 2Petr 2:9, 3:18.
Fil3:7-14, Math20:25-28, Yoh20:21, Gal5:22-25, Rum8: 38-39, 1Yoh4:4, Ebr10

12.Kanisa 
Kanisa ni jamii ya waumini wanaomkiri Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi katika
mfululizo wa kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za agano la kale, tunaitwa
kutoka katika ulimwengu, na tunajiunga pamoja kwa ajili ya ibada, kwa ajili ya ushirika, kwa
ajili ya mafundisho katika neno, na kwa ajili ya maadhimisho ya meza ya bwana, kwa ajili ya
huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni kote, kanisa
linapata mamlaka yake kutoka kwa kristo, aliye neno lililofanyika mwili, na kutoka katika
maandiko, ambayo ndiyo neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya Mungu, waliofanywa nay
eye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika misingi ya agano jipya. Kanisa ni mwili
wa Kristo, jamii ya weny imani ambayo kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi
ambaye kwa ajili yake kristo apate kulisafisha na kulitakasa.Wakati wa kurudi kwake kwa
ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewew kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne zote,
walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu na lisilo na
ila.(Mwa12:3, Mdo:7:38, Waef4:11-15, 3:8-11, Math28:19,20, 16:13-20, 18:18,
Waef19:22,23, 5:23-27, Wakol1:17-18).

13.Masalio na Utume Wake
Kanisa la ulimwengu lijumuisha wale wote ambao kwa kweli wanamwamini kristo, lakini
katika siku za mwisho, kipindi cha kuenea kwa ukengeufu, masalio wameitwa kuzishika
amri za Mungu na imani ya Yesu kristo. Masalio hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya
hukumu, hutangaza wokovu kupitia kristo, na hupiga mbiu ya kukarinia kwa marejeo yake.
Tangazo hili huwakilishwa katika mfano wa malaika watatu wa ufunuo 14, juambatana na
kazi ya hukumu mbinguni na kuwa na matokeo ya kazi ya toba na matengenezo duniani.
Kila muumini anatakiwa kuwa na sehemu binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni
kote. (Ufu12:17, 14:6-12, 18:1-4, 2Wakor 5:10, Yuda3,14, 1Petro1:16-19, 3:10-14,
Ufu21:1-14)

14.Umoja katika Mwili wa Kristo 
Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki wengi, walioitwa kutoka katika taifa, kabila, lugha,
na watu. Katika kristo tu viumbe wapya, ubainishi wa rangi, tamaduni, elimu, na taifa, na tofauti
kati ya tabaka ya juu nay a chini, tajiri na maskini, mwanaume na 
mwanamke,havipaswi kuleta mgawanyiko miongoni mwetu.Sote tu sawa katika kristo,
ambaye kwa roho mmoja ametufunga katika ushirika mmoja pamoja nay eye na sisi
wenyewe kwa wenyewe, tunapaswa kutumika na kutumikiwa pasipo kupendelea au kusita.
Kupitia kwa Yesu kristo katika maandiko tunashiriki imani na tumaini moja, na tunawafikia
wote kwa ushuhuda mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu
mmoja mwenye nafsi tatu, ambaye ametufanya sisi tu watoto wake.(War12:4,5,
1Wakor12:12-14, Math28:19,20, Zabr133:1, 2Wakor5:16,17, Mdo17:26,27, Waef4:14-16,
4:1-6, Yoh17:20-23)

15.Ubatizo 
Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu kristo, na
kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa maisha. Hivyo
tunamkubali kristo kuwa Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tunapokelewa kama
washiriki wa kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa muungano wetu na kristo, msamaha wa
dhambi zetu na kupokea kwetu Roho Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa najini na unategemea
uthibitisho wa imani katika yesu na ushindi wa toba ya dhambi. Unafuata mafunzo katika
maandiko matakatifu na ukubali wa mafundisho yake. (Warum6:1-6, Wakol2:12,13,
Mdo16:30-33, 22:16, 2:38,Math28:19-20)

16.Meza ya Bwana 
Meza ya Bwana ni ushiriki katika mfano wa mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa
imani katika yeye, Bwana na mwokozi wetu. Katika ushirika huu kristo anakuwepo
kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadri tunavyoshiriki, kwa furaha tunatangaza mauti
ya Bwana mpaka arudipo tena. Maandalizi kwa ajili ya meza ya Bwana hujumuisha kujihoji
nafsi, toba na ungamo. Bwana aliamua huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha
kutakaswa upya, kuonyesha nia ya kutumiana wenyewe kwa wenyewe katika unyenyekevu
ufananao na wa kristo, na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya Meza ya
Bwana wazi kwa waumini wote wakristo. (1Wakor10:16,17. 11:23-30, Math 26:17-30,
Ufu3:20, Yoh6:48-63, 13:1-17)

17.Karamu za Roho na Huduma 
Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho
ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya
kanisa na wanadamu. Zikitolewa kwa wakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila
mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa
na kanisa katika kuytekeleza shughuli zake zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na
maandiko huduma hizi hujumuisha huduma kama: Imani, uponyaji, unabii, mahubiri,
mafundisho, utawala, upatanisho, huruma, na huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya
msaada na faraja kwa watu. Baadhi ya washiriki huitwa na mungu na kukirimiwa na Roho
kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, na utume, na
huduma za kufundisha zinahitajika hasa katika kuwapatia zana washiriki kwa ajili ya
huduma kulijenga kanisa hadi ukomavu wa kiroho, na kukuza umoja wa imani na maarifa
ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu ya
mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa Mungu, nakujengeka imara
katika imani na upendo.(Warumi12:4-8, 1Wakor12:9-11, 27,28. Waef4:8,11, Mdo6:1-7,
1Petr4:10-11)

18.Karama ya Unabii 
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii, karama hii ni alama-kitambulisho cha
kanisa la masalio na ilidhihirishwa katika huduma ya Ellen G. White. Kama mjumbe wa
Bwana, maandishi yake ni chanzo kiendelezi na yenye mamlaka ya ukweli yanayolipatia
kanisa faraja, uongozi, mafundisho, na maonyo. Pia yanaweka wazi kuwa Biblia ndiyo
kanuni ambayo kwa hayo mafundisho yote na uzoefu lazima vipimwe. (Yoeli2:28,29,
Mdo2:14-21, Waeb1:1-3, Ufu12:17, 19:10)

19.Sheria ya Mungu
Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimetiwa pamoja katika Amri kumi na mfano wake
ulidhihirishwa katika maisha ya kristo,. Nazo zinadhihirisha upendo wa Mungu, mapenzi
yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti kwa
watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo msingi wa agano la Mungu na watu wake na
kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia uwakala wa Roho Mtakatifu zinasonda dhambi
na kuhamsha hisia za hitaji la mwokozi. Wokovu wote ni katika neema, na si kwa matendo,
lakini tunda lake ni utii wa amri kumi. Hutii huu hukuza tabia ya kikristo na huwa na
matokeo ya ustawi. Ni ushuhuda wa upendo wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya
wanadamu wenzetu. Utii wa imani udhihirisha uwezo wa kristokubadilisha maisha, na
hivyo huimarisha ushuhuda wa kristo. (Kut 20:1-17, Zab40:7,8 Math22:36-40 Kumb28:1-
14 Math5:17-20, War8:3,4 Zab 19:7-14)

20.Sabato 
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za uumbaji, alipumzika siku ya saba na kuanzisha
sabato kwa ajili ya watu wote kama kumbukumbu ya uumbaji. Amri ya nne ya sheria za
Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la sabato hii ya siku ya saba kama siku ya
mapumziko, ibada, na huduma kulingana na mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa
sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano yenye furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi. Ni
mfano wa ukombozi wetu katika kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu, na
mwonjo wa umilele wetu wa siku zijazo katika ufalme wa Mungu. Sabato na ishara ya daima
ya mungu ya agano la milele la Mungu kati yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa
wakati huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimishola
matendoya Mungu ya uumbaji na ukombozi. (Mwa 2:1-3, Kut20:8-11, Luka4:16, Isay56:5-
6, 58:13-14, Math12:1-12, Ezek20:12-20, Kumb5:12-15, Wal23:32, Marko1:32).

21.Uwakili 
Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa nay eye wakati na fursa, uwezo na mali, na
mibaraka ya dunia na raslikamali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi.
Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na kwa wanadamu wenzetu, na kwa kurudisha Dhaka na kutoa sadaka kwa ajili ya utangazaji wa injili yake na kwa
utegemezaji na ukuaji wa kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili
ya malezi katika upendo na ushindi dhidi yao choyo na tama. Wakili kufurahia mibaraka
inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake.(Mwa1:26-28, 2:15, 1Nyak29:14,
Hagai 1:3-11, Malak3:8-12, 1Wakor 9:9-14, Math23:23, 2Wakor8:1-15 Warumi15:26-27.).

22. Mwenendo wa kikristo
Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri, kujisikia, na kutenda kutenda kulingana na kanuni za
mbinguni. Ili Roho aumba ndani upya ndini yetu tabia ya Bwana wetu tunajihusisha tu
katika mambo yale ambayo yatazaa katika maisha yetu usafi unaofanana na kristo, afya, na
furaha katika maisha yetu. Hii inamaanisha kwamba maraha na maburudisho yetu
yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji na uzuri wa kikristo. Huku tukitambua tofauti
za kitamaduni, mavazi yetu yanapaswa yawe ya kawaida, si ya anasa, na safi, yanayostahili
wale ambao uzuri wao wa asili yake si mapambo ya nje, bali asili yake ni mapambo
yasiyoharibika, yenye roho ya upole na utulivu. Pia inamaanisha kwamba kwa kuwa miili
yetu ni maekalu ya Roho mtakatifu, tunapaswa kuitunza kwa akili. Pamoja na mazoezi
tosha na mapumziko, yatupasa kuchagua lishe yenye afya sana kadiri inavyowezekana na
kuepuka vyakula visivyo najisi, vilivyotajwa katika maandiko matakatifu. Kwa vile vinywaji
vya vileo, tumbaku na matumizi mabaya ya madawa hudhuru miili yetu, yatupasa
kuepukana nayo pia. Badala yake yatupasa kujishughulisha na chochote kile kitakacholeta
mawazo yetu na miili yetu yawe katika nidhamu ya kistro, ambaye hutamani uzima wetu,
furaha, na wema. (Warumi 12:1-2, 1Yoh 2:6, Waef5:1;21, Wafil 4:8, 2Wakor 10:5, 6:14,
7:1, 1Pet3:1-4, Walawi 11:1-47, 3Yoh. 2)

23. Ndoa na Familia 
Ndoa ilianzishwa Edeni na Mungu na ikasibitishwa na Yesu kuwa muungano wa maisha
yote kati ya mwanaume na mwanamke katika wenzi wenye upendo. Kwa mkristo kifungo
cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na kishirikiwe tu na wenzi wenye imani moja.
Upendo wa hiari, heshma, staha, na uwajibikaji ndizo fito za {kujenga}uhusiano huu,
ambao utaakisi upendo, utakatifu, ukaribu, uthabiti wa uhusiano kati ya kristo na kanisa
lake. Kuhusu talaka, Yesu alifundisha kwamba mtu anayemwacha mwenza, isipokuwa kwa
sababu ya uasherati, na akaoa {au kuolewa} na mwingine azini. Ingawa baadhi ya
mahusiano ya kifamilia huenda yakashindwa kufikia lengo, wenzi katika ndoa ambazo
wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa mwenzake katika kristo wanaweza kufaulu kufikilia
katika umoja wenye upendo kupitia uongozi wa Roho na malezi ya kanisa. Mungu hubariki
familia na anakusaidia kwamba washirika wake watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu
kamili. Wazazi wawalee watoto wao katika kumpendeza na kumtii Bwana. Kwa kielelezo
chao na maneno yao wawafundishe kwamba kristo ni mtiishaji mwenye upendo, daima
mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe kiungo katika mwili wake, familia ya Mungu.
Kukuza ukaribu wa mahusiano wa kifamilia ni moja wapo ya alama{ya kujulisha}ujumbe wa
mwisho wa injil. (Mwa 2:18-25, Math 19:3-9, Yoh 2:1-11, 2Wakor6:14, Waef5:21-33, Luka
16:18, 1Wakor7:10-11, Kut20:12, Kumb6:5-9, Mith22:6, Mal 4:5-6)

24. Huduma ya Kristo katika Hekalu la Mbinguni
Kuna hekalu mbinguni, hema la kweli lililosimamishwa na Bwana na siyo mwanadamu.
Ndani yake kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha kupatikana kwa ajili ya waumini
fanaka za kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote.
Alizinduliwa kuwa kuhani wetu mkuu na akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa
kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka 1884, mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku
2300, aliingia katika awamu ya pili nay a mwisho katika huduma yake ya upatanisho. Ni
kazi ya hukumu ya upelelezi ambaya ni sehemu ya mwisho ambayo hatimaye itakomesha
dhambi yote, iliyokuwa mfano wa kutakaswa kwa hekalu la kale la waebrania katika siku ya
upatanisho. Katika huduma hiyo kielelezo hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa
kafara, likini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamilifu ya damu ya Yesu.
Hukumu ya upelelezi kufunua kwa viumbe wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu
wamelala katika kristo na hivyo, katika yeye wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika
ufunuo wa kwanza. Pia inadhihirisha zazi ni nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani
ya kristo, wakishika amri za Mungu na imani ya Yesu, na katika yeye, hivyo basi, wako
tayari kwa ajili ya kuhamasishwa kuingia katika ufalme wa milele. Hukumu hii huthibitisha
haki ya Mungu, katika kuwokoa wale wanaomwamini Yesu. Hutangaza kwamba wale
waliohudumu kuwa watiifu kwa Mungu watapokea ufalme. Hitimisho ya huduma hii ya
kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufunga mlango wa rehema ya mwanadamu kabla ya
marejeo ya Yesu. (Waebr 8:1-5, 4:14-16, 9:11-28, 10:19-22, 1:3, 2:16-17. Dan 7:9-27, 8:13-
14, 9:24-27. Hes 14:34. Ezekl 4:6 Ufu 14:6-7, 20:12, 14:12, 22:12. )

25. Kuja kwa Kristo mara ya pili 
Kuja kwa kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la kanisa, hitimisho kuu la injili.
Kuja kwa mwokozi kutakuwa halisi, binafsi, kutaonekana kwa dunia mzima. Atakaporudi
wenye haki waliokufa watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu
na kuchukuliwa kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa
sehemu nyingi za unabii, pamoja na hakli ya sasa ya ulimwengu, huonyeshe kwamba kuja
kwa kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi
tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote. .(Tito 2:13, Math 24, Mdo1:9-11, Math24:14,
Ufu1:7, 14:14-20, Math24:43-43, Wakor15:51-50, 1Wathes1:7, 4:13-18, 5:1-6, Marko 13,
Luka 21:2, Tim 3:1-5).

26. Mauti na Ufunuo
Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yakehapatwi na mauti,
atawapa uzima wa milelewaliokombolewa wake. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya
kutokuwa na fahamukwa watu wote. Wakati kristo, aliye uzima wetu, atakapotokea, wenye
haki waliofufuliwa na walio hai watafikwa utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki Bwana
wao. Ufufuo wa pili ambao ni ufufuo wa waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye.
(Warum 6:23,1Tim 6:15-16, Mhu 9:5-6, Zab 149:3-4, Yoh 11:11-14, 1Wakor 15:51-54,
1Wathes 4:13-17, Ufu 20:1-10)
.
 27. Milenia {Miaka Elfu} na Mwisho wa Dhambi
Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati
ya ufufuo wa kwanza na pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa, dunia itakuwa
ukiwa na utupu, bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika
zake. Mwishowe kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni.
Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na shetani na malika zake watauzingira
mji, Lakini moto kutoka mbinguni utawateketeza ili kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu
utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele. (Ufu 20, 1Wakor 6:2-3, Yer 4:23-26,
Ufu 21:1-5,Mal 4:1, Ezekl 28:18-19)

28. Dunia Mpya
Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa,Mungu ataweka tayari makao ya milele
waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na
kujifunza mbele zake. Kwa hapa Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu
na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakuwepo
tena. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo, naye
atatawala milele. Amina. (2Pet 3:13, Isa 35, 65:17-25, Math 5:5, Ufu 21 :1-7, 22:1-5, 11:5).

Sabbath Time | Muda wa Sabato

Place: Dar es Salaam, Tanzania

Start: 06:17 PM, 04/26/2024

End: 06:17 PM, 04/27/2024

Live Media | Tazama live

Copyright ©2015 Sinza Seventh day Adventist Church
Designed By GE Male M