Kanisa la Waadventista wa Sabato Sinza
Kanisa la Waadventista wa Sabato Sinzai ni jumuiya ya watu wa imani ya Kikristo tunaoshika Sabato Takatifu na kumwabudu Mungu wa Mbinguni kwa pamoja tukiwa ni sehemu ya maelfu ya makusanyiko ya waadventista wenzetu nchini Tanzania na ulimwenguni kote. Ni Kanisa linalosisitiza na kuandaa ulimwengu juu ya ukio wa pili wa Yesu Kristo tukisema Yesu anakuja Upesi. Washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Sinza hukusanyika kumwabudu Mungu kila siku ya Jumamosi katika jengo la ibada lililopo eneo la Sinza Madukani, mita 300 kutoka barabara ya Shekilango, karibu na Namnani Hotel. Kati ya makundi yaliyoanzishwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Manzese mojawapo ni kundi lililokuwa likiabudu katika shule ya Msingi Mugabe na kuitwa kundi la Mugabe. Mwaka 2008 kundi la Mugabe lilitengwa rasmi kuwa Kanisa na kupewa jina la "Kanisa la Waadventista wa Sabato Sinza".
Kwa sasa Kanisa la Waadventista wa Sabato Sinza lina jumla ya washiriki waliobatizwa 253.