MSIMAMO WA KANISA JUU YA NEMBO YAKE NA MAELEZO JUU YA KILE KINACHOWAKILISHWA.
FALSAFA YA NEMBO
Nembo ina utambulisho na, kama unavyotambua, utambulisho ni chochote ambacho wewe au wengine wanachoweza kutengeneza ili kiwe. Kitambulisho hicho ni kitufulani ambacho kinatengenezwa kutokana na hadhi na wakati. Hata hivyo, kwa nembo ili iwe mali ya kundi maalumu, ni lazima ilindwe kisheria na kutambuliwa na hivyo ndivyo inavyotokea kuwa, nembo lazima iwe ya kipekee na yenye msimamo.
Mojawapo ya matatizo ambayo kanisa limekabiliana nayo kwa miaka mingi iliyopita, imekuwa ni kwamba kamwe halijawa na nembo yake ya kipekee na yenye msimamo; kwa uhakika kamwe hapajakuwa na makubaliano au utwaaji wa nembo kiofisi ya aina yeyote. Hatimaye michoro mingi wakilishi imekuwa inatumika kama nembo kwa vyombo mbalimbali vya kanisa kama vile malaika 3 na Dunia na tarumbeta. Tofauti hizi zote katika maeneo mbali mbali zimekuwa zikitumiwa na makundi ya kanisa na makundI mengineyo. Na kwa sababu hapakuwa na msimamo na hata ulindwaji wa kisheria, hatukuweza kuimiliki au kutawala kwa matumizi ya michoro hii dhidi ya watumiaji wengine. Kujibu (kutatua) tatizo hilo, ilitulazimu kutengeneza nembo ambayo ina upekee na msimamo madhubuti.
UUNDWAJI WA NEMBO (LOGO DEVELOPMENT).
Kwa kuwa tulikuwa tunaanza kuanzia chini (kwangua chini), tuliajiri Mtaalumu wa Kiadventista (mbunifu wa Kiadventista) na kutafiti mawazo ambayo yatawakilisha kanisa, utume wake, imani yake, na vilevile kuakisi ulimwengu wa leo katika hali ya mtizamo na hisia. Matokeo unayoyaona ni baada ya mchakato mzima (hatua zote) wa kawaida wa kanisa wa kamati nyingi za mara kwa mara, mapitio na kura za kanisa katika mkutano wa mashauri. (Jambo)Halikufanyika hewani, bali ni jambo la watu wengi kutoka duniani kote likijumuisha michango mbalimbali na uthibitishwaji.
MAANA YA NEMBO
Baadhi ya watu wamelaumu kwamba uondoaji (kuachwa) kwa nembo ile ya “zamani” inawakilisha kuachana na kile tunachokiamini, ni miongoni mwa malaumu. Hakuna kinachoweza kuwa mbali na ukweli. Hatuakisi kutoka kwenye nembo yetu; nembo yetu inatuakisi sisi (tulivyo sisi), na ikiwa tupo sahihi kwa kile tunachokiamini, hicho ndicho nembo yetu itasimama kwacho (itawakilisha). {Nothing could be further from the truth. We don't reflect our logo; our logo reflects us, and if we are true to what we believe, that is what the logo will come to stand for}. Kwa uhalisi wa jambo hili nembo mpya kwa ukamilifu zaidi inawakilisha kwa mapana ya kile tunachokiamini. Inaanza na msingi wa Neno, wenye kiini cha Msalaba, njia ya Wokovu wetu; ikionesha miali mitatu inayozunguka Dunia, ikiwakilisha kwa pamoja Utatu Mtakatifu [ Baba, Mwana, Roho Mtakatifu] na vilevile ujumbe wa malaika watatu kwa ulimwengu wote. Na yote haya yameoneshwa kwa njia rahisi, na bado kwa usanifu na mtindo wa kisasa. MWISHO WA TAFSIRI.
“Huu uthibitisho wa kile kilicho halisi na sio kile kisicho halisi” na mch. Mwanga.
NI MSIMAMO WA KANISA LA WAADVENTISTA ULIMWENGUNI JUU YA NEMBO YAKE YA UTAMBULISHO ULIOTOLEWA NA GENERAL CONFERENCE DHIDI YA TAFSIRI POTOFU YA KILE AMBACHO SICHO HALISI.
NA KUTAFSIRIWA